Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu limetoa taarifa katika kumbukumbu ya mwaka wa pili wa kuuwawa kishahid Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, huku likiitaja njia ya Sayyid wa Muqawama kuwa ya milele, na damu yake safi kuwa chemchemi inayobubujika ya nguvu ndani ya mwili wa Muqawama, pamoja na kuinuliwa heshima na fahari ya Hizbullah na Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon.
Sehemu ya taarifa hiyo inasema: Miaka miwili imepita tangu siku ile ya umwagaji damu na jinai ya kikatili na ya kigaidi; siku ambayo mkono wa kihalifu wa utawala wa kishetani wa Kizayuni uliunyang’anya Muqawama wa Kiislamu, hususan Hizbullah shujaa wa Lebanon, Sayyid wa Muqawama, mbeba bendera ya uhuru, Hujjatul-Islamu wal-Muslimina Sayyid Hassan Nasrullah. Lakini kinyume na dhana na nia ovu za adui, mwangaza wa damu yake takatifu haukuzimika, bali umegeuka kuwa chemchemi inayobubujika ya nguvu na ustawi ndani ya mwili wa Muqawama, na kuwa wa milele.
Taarifa hiyo imeongeza: Sayyid Hassan Nasrullah hakuwa kiongozi tu; alikuwa mbunifu wa kimkakati wa Muqawama wa kisasa, mwanamkakati wa uwanja wa vita na diplomasia, na mfano halisi wa uhusiano usiokatika kati ya mataifa yanayopinga utawala wa mabavu katika eneo hili. Kwa kumfuata Mola na kiongozi wake, Imam Khamenei shahidi (Mwenyezi Mungu autukuze utajo wake), aliuinua Muqawama kutoka kuwa mbinu ya mapambano na kuufanya kuwa mfumo wa fikra, utambulisho na ustaarabu, na akathibitisha kwamba Muqawama si mwitikio tu, bali ni chaguo la kimkakati na mfumo wa maisha wenye heshima na unaozalisha nguvu.
Taarifa hiyo inaendelea kwa kueleza kwamba; Sayyid mtukufu na mpiganaji wa Muqawama, akiwa katika kilele cha ushujaa, ukweli, ufasaha na uthabiti wa kipekee, maneno yake yalitikisa milima na kuangaza nyoyo; na kusema: Ushawishi wa Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah ulikuwa umevuka mipaka ya eneo; na mwangaza wake kutoka Lebanon na Palestina hadi Yemen, Iraq, Syria na maeneo mengine, ulikuwa umegeuka kuwa sauti ya dhamiri iliyoamka ya Umma wa Kiislamu.
Taarifa hiyo imesisitiza: Shahidi Nasrullah aliamini kwamba Muqawama ni uwanja mmoja wenye umoja, na kwamba ushindi katika sehemu yoyote ya uwanja huu ni ushindi kwa wote.
Taarifa hiyo imeongeza: Bila shaka, kipindi cha uongozi wa Shahidi mtukufu Sayyid Hassan Nasrullah ni kipindi chenye kung’aa zaidi na chenye fahari kubwa zaidi katika historia ya Lebanon yetu pendwa, na nafasi yake ya kipekee katika historia ya kisasa ya eneo hili ni ya nadra na ya kudumu. Jina lake katika mfumo wa fikra wa Muqawama daima litatambuliwa kama la mwanamkakati na mtaalamu wa nadharia aliyeutoa Muqawama kutoka pembezoni na kuuleta katikati, na kuugeuza kuwa mfumo wa fikra uliotawala katika hesabu za eneo. Aidha, hadi wakati wa kuuwawa kwake kishahidi, aliweka uwiano wa kuzuia mashambulizi dhidi ya utawala wa Kizayuni na kuangusha milele ngano ya kwamba utawala huo hauwezi kushindwa.
Katika kuendelea, taarifa hiyo imesisitiza: Bila shaka, njia ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah itaendelezwa na Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon pamoja na wapiganaji wa Hizbullah chini ya uongozi wa mrithi wake mwadilifu, Hujjatul-Islamu wal-Muslimina Sheikh Naim Qassem, katika kilele cha utukufu, heshima na nguvu; kama ambavyo Muqawama wa kipekee wa kusini, pamoja na ushujaa na mashujaa wa matukio ya kihistoria huko Ali al-Tahir, unatoa ishara ya kusambaratika utawala wa Kizayuni.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa: Leo, mbele ya Muqawama katika eneo lote, hususan tangu kutokea vita vya kulazimishwa vya siku 12 na siku 40 vilivyoendeshwa na Marekani ya kigaidi na utawala bandia wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, imeonesha kwamba ni alama ya heshima, uhuru, kusimama imara dhidi ya utawala wa mabavu na dhidi ya ukaliaji wa ardhi.
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, mwishoni mwa taarifa hiyo, huku likiifanya upya ahadi ya utiifu kwa Maimamu Wakuu wawili na Shahidi wa Mapinduzi, na kuheshimu malengo ya juu ya mashahidi wa Muqawama, hususan mashahidi “Sayyid Hassan Nasrullah” na “Jenerali Mkuu wa Walinzi, Abbas Nilforoushan”, limeeleza kwamba: Udhibiti, uangalizi na uendeshaji wa Muqawama mikononi mwa wapiganaji shupavu wa Uislamu katika lango la kimkakati la “Hormuz”, katikati ya mapambano ya sasa ya ustaarabu na uwepo, ni miongoni mwa mafanikio yanayotokana na imani na kuamini msaada wa Mwenyezi Mungu.
Aidha, imesisitiza: “Kwa mara nyingine, kwa sauti kubwa na katika kilele cha uthabiti na nguvu, tunatangaza: Kuutetea Muqawama, kutetea haki za wanyonge, na kusimama imara hadi kukombolewa kikamilifu Quds Tukufu, ni jukumu la milele, la kitaifa na la kibinadamu la Jeshi la Walinzi lenye nguvu, la wananchi na la kimapinduzi, pamoja na vikosi vingine vya ulinzi vya nchi. Na kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, chini ya uongozi wa Amiri Mkuu wa Vikosi Vyote vya Ulinzi, Ayatullah Imam Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei (Mungu azidishe kivuli chake), na kwa uongozi wa utukufu na nguvu wa wananchi wa Iran, pamoja na umoja wa nyanja zote, njama za Shetani Mkuu, Marekani ya kigaidi, na mbwa wake mkali, utawala wa Kizayuni unaokalia ardhi na waungaji mkono wake, hazitawahi kufanikiwa. Wapiganaji wa Uislamu wataandika historia ya mustakabali na hawatarudi nyuma hata hatua moja hadi ushindi wa mwisho.”
Maoni yako